This audio is part of the interview that I made in Gaborone at Kezilahabi's place. I was his guest for circa 10 days (thanks to him and his family). The interview lasted circa 3 hours, I used circa one third of it for my book on him "The voice of the text and its body. The continuous reform of Kezilahabi’s poetics. Cologne: Rüdiger Köppe Verlag. (2019).
I am so grateful to have had the privilege of knowing him but above all for his writings, which are acute living thought and poetry.
kwa heri mwalimu wangu
tangu leo utashindwa
kubadilikabadilika
kubadilishabadilisha
sote hushangaa ulivyopenda
macho yako yakacheka mzaha
yalikutanaga yangu na yako
asante kutushangaza
utuvumilie hatujaelewa vizuri
tutaendelea kutafakari
tutaendelea kuficha mawazo yako
tutaanza kukuenzi kuficha mawazo yako
ili uwe kanuni bila hatari yoyote
bila ukweli bila uhuru
bila wajibu usiathiri
vijana usiathiri maneno
yetu hadharani
au kifo chako kitafungua mlango uelekeao
katikati ya ujuzi na urazini mpya?
mwalimu wangu muda umefika
budi wameshaimba zaidi ya mwaka
kilio chako
kutoka sasa kitakuwa kwenye sauti zetu
zinazopanda zinazovunja zinazounga
kuwapo kwako ulituhakikisha
dhidi ya ukawaida
unaotubana ndani ya wavu wa kila siku
kila uzi wake tumeshaufahamu
ulikuwa ule wa kitambaa
ambacho mama alitubembeleza
maji yavuka nyuzi mpaka Nili
mbali mpaka Mediterraneo
Nabili inatiririka kutokana na wakati
uhuru wake tutaelewa mkondo na wakati
kutokana na uwezo na uhuru wetu
kutambua kung’amua ni ngumu sana
urazini mpya haujaja
ila utuvumilie mwalimu wangu
wakati fulani utafika mtiririko wako
utamwangilia miwili yetu
boga litaota palepale
litaparamia parapara
tutakuonaga kila wakati ujao
(Roberto Lumuli Gaudioso)
Тэги:
#Afrika #Kezilahabi #kiswahili #fasihi #swahili #falsafa #philosophy